Sunday, November 10, 2019

WAKE WA VIONGOZI WASHEREKEA MAULID NA WATOTO WA BUHANGIJA


WAKE wa Viongozi wamesherehekea sikukuu ya Maulid kwa kutoa zawadi ya vitu mbalimbali pamoja na kula chakula cha mchana na watoto wa Kituo cha Watoto Wenye mahitaji maalumn cha Buhangija mjini Shinyanga.

Akinamama hao ambao ni wanachama wa kikundi cha Millenium Women Group, walitoa zawadi hizo jana (Jumapili, Novemba 10, 2019). Zawadi walizozitoa kwa watoto ni pamoja na nguo, sabuni, vinjwaji baridi, madaftari, kalamu na taulo za kike.

Wanawake hao waliongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa yaliyojengwa na kikundi hicho pamoja na matundu ya vyoo 10.
  
Baadae wake hao wa viongozi wakiongozwa na Mlezi wao Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na Mwenyekiti wao, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda walicheza muziki na watoto jambo ambalo liliwafurahisha sana watoto.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko na viongozi wengine wa Chama tawala CCM pamoja na viongozi wa Serikali wa mkoa wa Shinyanga.


 (mwisho)


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.