Afya Moja ambayo ni dhana
inayojumuisha sekta ya Afya ya binadamu, Mifugo, Wanyamapori na Mazingira
katika kujiandaa, kubaini, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri sekta
hizo, hivi karibuni umezinduliwa Mradi wa kimkakati wa kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya binadamu na wanyama hususan Sokwe, ujulikanao kama Bush to Base, mradi huo
utatekelezwa mkoani Kigoma katika Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa 18 vijiji
vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa milima
ya Mahale.
Lengo la mradi huo unaosimamiwa na kuratibiwa
na shirika lisilo la kiserikali la Bush-To-Base
(B2B), ni kuongeza
kasi ya ushirikiano kati ya Wizara za Kisekta na kuongeza uelewa wa dhana ya
Afya Moja miongoni mwa wataalamu na wadau wengine wa sekta za afya ya wanyama,
binadamu, kilimo na mazingira ili kuwa na mikakati shirikishi ya uchunguzi,
utambuzi na udhibiti wa magonjwa.
Akiongea wakati wa kuzindua
Mradi huo mkoani Kigoma, Katibu Tawala wa mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta
alifafanua kuwa Mradi huo ni muhimu katika kuimarisha
usalama wa afya ya wananchi wa mkoa wa Kigoma na taifa kwa ujumla kwa kuwa Kume kuwa na mwingiliano mkubwa kati ya watu na wanyama katika mazingira yao hivyo dhana dhana ya afya moja haina budi kutumika kwakuwa ni
utaratibu ulioratibiwa kwa kushirikisha sekta zote za Afya.
“Kwa kuwa tafiti zinabainisha kuwa
vimelea
vingi vinavyo sabababisha magonjwa kwa binadamu zaidi ya 60% vinatoka kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi
yanatokea pale binadamu anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari,
hatuna budi kuongeza ushirikiano na mawasilaino katika nyanja
za afya ya binadamu, wanyama na mazingira ili kuwa na ufanisi katika kudhibiti
magonjwa yanayoambukiza” alisistiza Mchatta.
Kwa
upande wake Rais wa shirika lisilo la kiserikali
la Bush-To-Base
(B2B), Dkt Teresa Sylvin amefafanua kuwa mradi huo unajikita
katika matokeo ya tafiti za kisayansi kuhusu afya ya Sokwe katika Hifadhi ya
Taifa milima ya Mahale ambazo amezifanya kwa zaidi ya miaka 25.
“Kimsingi huu mradi unakusudia kutumia dhana ya
afya moja kwa kutumia matokeo ya tafiti ili kuweza kuzishirikisha sekta za afya
ya wanyama, binadamu, kilimo na mazingira ili kuwa na mikakati shirikishi
ya uchunguzi, utambuzi na udhibiti wa magonjwa yatokanayo na Sokwe kwenda kwa
binadamu. Lakini tunalenga kuishirikisha jamii ambayo inaishi katika mazingira
ya mradi huu, naamini kwa kutumia afya moja tutafanikiwa ” alisema Dkt.Teresa
Mradi
huo utakaotekelezwa kwa miaka mitatu mkoani Kigoma utakuwa ukifanya kazi za
uratibu kwa kushirikiana na Ofisi yaWaziri Mkuu, Kupitia Dawati la Afya moja,
tayari umepata ufadhili kutoka serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa Sayansi
na mwingine unajihusisha na Samaki na Wanyamapori.
MWISHO.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.