Wednesday, January 9, 2019

MAMA WADOGO WILAYA YA KALIUA WAPEWA ELIMU YA STADI ZA KUJITAMBUA

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora, Mhe. Abel Busalama, akifungua mafunzo kwa Mama wadogo (Young Mothers) ya kujitambua, malezi ya familia, Afya na lishe, Kilimo biashara, Ujasiriamali, kuunda vikundi vya uzalishaji mali na kuwaunganisha kwenye fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi. (Kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe akielezea jambo kwa Mama wadogo (Young Mothers) kuhusu Programu hiyo ya Kitaifa inayolenga kuwawezesha mama wadogo kupata mbinu na stadi za kujitambua, uthubutu, kufanya maamuzi sahihi na kujiwekea malengo katika maisha yao.

Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Dorah Meena akiwasilisha mada kuhusu kujitambua kwa Mama wadogo (Young Mothers) walioshiriki mafunzo hayo ukumbi wa Mt. John Paul II, uliopo Wilaya ya Kaliua.

Mwezeshaji kutoka Benki ya NMB, akitoa mada kuhusu Mikopo na Akaunti za kibenki zinazotolewa na benki hiyo.

Baadhi ya Mama wadogo (Young Mothers) wakifuatilia mada kuhusu Malezi ya Familia iliyokuwa ikiwasilishwa na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Kaliua Bw. Manase Satiel.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Abel Busalama (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mama wadogo walioshiriki mafunzo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Idara ya Maendeleo ya Vijana). Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.