NA.
MWANDISHI WETU
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama amewataka watendaji wa kiwanda cha Viatu na bidhaa za ngozi
cha Karanga Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro kuzalisha bidhaa zenye ubora na
kuendana na Soko lililopo nchini.
Ametoa
kauli hiyo alipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki ili kukagua shughuli
za uendeshaji wa kiwanda hicho na kujiridhisha na ubora wa bidhaa zinazozalishwa.
“Niwatake
watendaji kuweka mikakati madhubuti ya kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora
kwa kuzingatia viwango vinavyotatiwa”, Mhagama
Aidha
Waziri aliwaasa watendaji wa kiwanda hicho kuendelea kutatua changamoto zinazowazunguka
za kimfumo kwa kuzingatia sheria na taratibu za uendeshaji wa kiwanda hicho ili
kuendana na ukuaji wa teknolojia na ushindani ulipo.
“Nisingependa
kuona kiwanda kinakwama kuzalisha bidhaa zenye ubora, hivyo ni vyema kuzingatia
sheria na kanuni za uendeshaji wa kiwanda katika ufanisi wa hali ya
juu”,alisisitiza mhagama.
Waziri alieleza
kuwa, ili kuwa na wateja wa uhakika ni vyema kutumia mbinu za kujitangaza juu
ya shughuli na bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia vyombo vya habari ili kuendana
na soko lililopo nchini.
Aidha
waziri alieleza Mpango mkakati wa ujenzi wa kiwanda kikubwa
cha Taifa katika eneo hilo la Gereza la Karanga na tayari eneo limetengwa kwa ajili
ya ujenzi na kuboresha kiwanda kilichopo ili kuongeza uzalishaji kwa wakati na
ubora unaotakiwa.
“Uwekezaji unalenga
kuboresha kiwanda cha zamani kutoka kuzalisha pair 150 kwa siku na kuzalisha pair
400 kwa siku ingawa mpango mkakati uliopo ni kuwa na kiwanda kikubwa kitakachozalisha
pair 4000 kwa siku”,alisisita Waziri
Mhagama.
Naye Kaimu Mkuu wa Kiwanda hicho,
Shalua Magandi alibainisha faida zinazotarajiwa kutokana na mradi wa kiwanda hichi
ni pamoja na uzalishaji wa ajira 5000 za
moja kwa moja na zaidi ya ajira 4000 kutokana na shughuli za uzalishaji nchini,
kuongeza Kodi kwa Manispaa, kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ngozi, kuongeza
manufaa kwa mkoa pamoja na mikoa inayozunguka kwa kuboresha mfumo wa maisha na
kuongeza kipato kwa wananchi.
Kwa upande wake Afisa
masoko wa kiwanda hicho Bw. Fredrick Njoka aliwataka Watanzania kuendelea
kununua viatu vinavyotengenezwa kwa bidhaa za ngozi kwa kuzingatia ubora na bei
nafuu kwa kuwa kiwanda hicho kinatumia mashine za kisasa kutoa nchini Italia ambao
ndiyo wenye ujuzi wa hali ya juu na teknoloji ya kisasa ya utengenezaji wa
mashine hizo.
“Wananchi msiogope
kututembelea na kununua bidhaa zetu kwa kuzingatia zina ubora wa na bei nafuu,
na tunapokea mahitaji ya kila aina kulingana na uhitaji wa wateja wetu”,alisema
Njoka
Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alieleza namna
watakavyotekeleza maagizo ya waziri pamoja na kuhakikisha usimamizi mzuri wa
shughuli za serikali.
“Nikushukuru kwa ziara yako
inatukumbusha kuendelea kusimamia utendaji wenye tija kwa watumishi wa Serikali
pamoja kuhakikisha kiwanda hiki kinazalisha bidhaa bora na kulingana na
mahitaji ya wateja”, alisema Warioba
Kiwanda
cha viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi kilizinduliwa rasmi Juni 3, 1977 na
Rais wa awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa
Taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere.Awali kilikuwa na ubia na Mfuko wa
hifadhi ya jamii wa PPF ambapo baada ya mabadiliko ya kuunganishwa kwa mifuko
hiyo , kwa sasa kina ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.