Sunday, January 13, 2019

UJENZI WA OFISI YA WAZIRI MKUU KWENYE MJI WA SERIKALI, IHUMWA DODOMA WASHIKA KASI.

Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji wa Serikali, Ihumwa, linaloendelea kujengwa na Mkandarasi  Mzinga Holding Company, tarehe 13 Januari, 2019, Dodoma.

Mmoja wa mafundi wa Mkandarasi Mzinga Holding Company, akijenga sehemu ya ukuta wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu, katika mji wa serikali, Ihumwa  Dodoma,   tarehe 13 Januari, 2019.

Katibu Mkuu Wizara ya  Ulizi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka akikaribishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Nigel Msangi, alipofika kukagua shughuli za Mkandarasi Mzinga Holding Campony, anayejenga jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji wa serikali Ihumwa Dodoma.,   Mkandarasi huyo yupo chini ya Wizara ya Ulizi, mwingine ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA-JKT, Kanali Rajab Mabele, tarehe 13 Januari, 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Ulizi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka akipata maelezo kutoka kwa Mratibu Ujenzi jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu wa  Mkandarasi Mzinga Holding Company, Kapteni, Erick Siara wakati alipofika  kukagua shughuli za Mkandarasi huyo katika mji wa serikali, Ihumwa , Dodoma, Mkandarasi huyo yupo chini ya wizara ya Ulizi,   tarehe 13 Januari, 2019.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.