Wednesday, August 16, 2017

WAZIRI MKUU AELEKEA NCHINI CUBA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika uwanja wa ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo 16 Agosti,2017 akiwa anaelekea nchini Cuba kwa ziara ya kikazi.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumatano, Agosti 16, 2017) kuelekea nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Akiwa nchini Cuba Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za afya, elimu utalii na Kilimo.

Aidha, nchi ya Cuba ni mojawapo ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.