WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea na kujionea mtambo wa kisasa wa kusafisha dhahabu kwa asilimia 99 unaomilikiwa na kampuni ya Sunshine Group
uliopo katika kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Ametembelea mtambo huo leo (Jumanne,
Agosti 1, 2017) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya na kusema
kuwa mtambo huo ni wa kwanza kuweza kusafisha dhahabu kwa kiwango hicho hapa
nchini.
Amesema kwa Tanzania kampuni ya Sunshine
Group ndiyo yenye mtambo wa kuweza kusafisha dhahabu na kufikia asilimia 99
ukilinganisha na makampuni mengine yanayomiliki migodi.
Pia Waziri Mkuu amesema Serikali
inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza
katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza kusafirisha
dhahabu halisi.
Naye Ofisa Madini Mkoa wa Mbeya,
Mhadisi Said Makwama amesema dhahabu inayosafishwa katika mtambo huo ikipelekwa
nje ya nchi inaingizwa sokoni moja kwa moja tofauti na migodi mingine.
Mhandisi huyo alisema Sheria mpya ya Madini imesaidia Serikali kupata kodi ya
juu itokanayo na Mrabaha wa asilimia 6 na ‘clearance and inspection fee’ ya
asilimia moja ya thamani ya madini
yanayosafirishwa ukilinganisha na mrabaha wa awali wa asilimia nne.
“Uzalishaji uliofanyika kwa mwezi Julai
tu Serikali imepata mrabaha wa sh. milioni 333 ukilinganisha na sheria ya
zamani Serikali ingepata shilingi milioni 191. Sheria mpya imewezesha Serikali
kupata mapato zaidi ya sh. milioni 142. Awali ilikuwa inapata sh. milioni 191 kwa gramu 52. 518 kwa mgodi
mmoja wa Sunshine.”
Kwa upande wake mbunge wa Chunya,
Mheshimiwa Victor Mwambalaswa ameiomba Serikali kukubali maombi ya Kampuni ya
Sunshine ya kujenga mtambo wa kuchenjulia mabaki ya mchanga wa dhahabu wilayani
Chunya ili kuweza kuongeza fursa za ajira, ambapo Waziri Mkuu amesema suala
hilo linashughulikiwa.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Sunshine Group Bw Leo Le alisema kampuni ya Sunshine Group ni ni miongoni mwa
makampuni makubwa kutoka nchini China yaliyowekeza Tanzania, ambapo thamani ya
uwekezaji wao ni zaidi ya Dola za Marekani milioni 100.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.