WAZIRI
 MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya 
mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.
Aliyasema hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.
Alisema
 kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko  ya 
mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.
“Kupitia
 Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa 
nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao 
wanayolima.”
Alitoa
 mfano wa zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na 
wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.
“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo.”
Alisema
 kufanikiwa kwa Soko la Bidhaa na Mfumo wa stakabadhi ghalani 
kunategemea sana msaada wa Serikali.  “Soko la Bidhaa la Ethiopia 
linalotajwa sana kwa mafanikio, limefikia malengo yake kutokana na mkono
 wa Serikali.” 
 Bw.
 Malekano alisema kutokana na umadhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano 
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wanamatumaini makubwa kwamba 
soko hilo  litatimiza malengo yake.
 
 
 
 
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.