Thursday, October 24, 2019

OFISI YA WAZIRI MKUU YATEMBELEA MIRADI YA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA –LIC WILAYANI KAKONKO

Mkulima wa zao la mpunga katika Wilaya ya Kakonso Bw. Silveter Mtondo ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Local Investment Climate (LIC)) akiwaonesha Timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Biashara namna kifaa cha palizi ya mpunga kinavyotumika walipotembelea katika Wilaya hiyo.
Kaimu Mkurugugenzi wa Wilaya Kakonko Bw. Christopher Bukombe akizungumza na timu kutoka Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kutoka  Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na watendaji wa TNBC walipotembelea kukagua na kujionea utekeleza wa miradi hiyo Oktoba 24, 2019 Mkoani Kigoma.
Timu ya wagakuzi kutoka Kitengo cha ukaguzi wa ndani Ofisi ya Waziri Mkuu na watendaji wa Baraza la Taifa la Biashara wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Local Investment Climate (LIC)) Bi.Imelda Hokororo akitoa amelezo kuhusu Kituo cha Biashara kilichojengwa na Taasisi hiyo Wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma, timu hiyo ilitembelea kukagua utekelezaji wa miradi hiyo Oktoba 24, 2019
Muonekano wa Jengo la Kituo cha biashara lililojendwa kwa ufadhili wa Mradi wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Local Investment Climate (LIC)) unaoratibiwa na Baraza la Taifa la Biashara lililopo Wilaya ya Kakonko mkoa wa Kigoma.
Mkaguzi wa ndani kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Omari Saidi akikagua na kuchukua taarifa za mashine ya kukoboa mpunga iliyojengwa kwa ufadhili wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Local Investment Climate (LIC)) wakati wa ziara ya kitengo hicho kuona utekelezaji wake wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma.


Afisa Biashara ambaye ni Mratibu wa LIC Wilaya ya Kakonko Bi. Imelda Hokororo akitoa maelezo kuhusu ofisi za Kituo cha Biashara (LIC) kwa watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na TNBC walipotembelea kukagua kituo hicho katika Wilaya hiyo.
Timu ya wagakuzi kutoka Kitengo cha ukaguzi wa ndani  Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na watendaji wa Baraza la Taifa la Biashara pamoja na watendaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kakokso wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jingo la mashine ya kukobolea mpunga lililojengwa kwa ufadhili wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara mkoani Kigoma.EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.