Monday, June 10, 2019

MAJALIWA AFUNGUA MICHEZO YA UMISETA KWENYE UWANJA WA NANGWANDA MJINI MTWARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka  mkoa wa Tanga wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Juni 10, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara kufungua michezo ya UMISETA kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Juni 10, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanamichezo wakati alipowasili kwenye uwanja wa Nangwada Sijaona mjini Mtwara kufungua Mashindano ya UMISETA, Juni 10, 2019. Wengine Pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelsius Byakanwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Simuyu wakiingia kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kushiriki katika Ufunguzi wa Michezo ya UMISETA uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 10, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya soka ya mkoa wa Mtwara wakati alipofungua mshindano ya UMISETA  kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Tanga Juni 10, 2019EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.