NA.MWANDISHI
WETU – OWM
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuka ameutaka
uongozi wa kiwanda kinachotengeneza bidhaa za cha za jasi (Gypsumboard) cha KNAUF kuendelea kushirikiana na jamii
inayowazunguka katika kujiletee maendeleo.
Ametoa kauli hiyo mapema
mwishoni mwa wiki hii alipotembelea kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ili kukagua shughuli za uzalishaji
zinazoendela pamoja na kusikiliza changamoto za wawekezaji hao na kuweza
kujadili masuala ya kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji
nchini.
Waziri Kairuki aliwataka
kuona umuhimu wa kuchangia katika shughuli za kimaendeleo katika maeneo
yanayozunguka kiwanda hicho hususan katika uboreshaji wa miundombinu na utoaji
wa misaada itakayofikia jamii kwa sehemu kubwa na si mtu mmoja mmoja ili kuleta
maendeleo katika eneo kubwa na kuondoa tofauti kubwa za kimaendeleo
zisizoendana na maendeleo ya maeneo kiwanda hicho.
“Ni muhimu sana, na ni
busara kuona ni kwa namna gani
mnashirikiana na wananchi wanaozunguka eneo hili katika kuleta maendeleo ili
kuhakikisha mnakubalika , na kuleta maendeleo ya eneo husika na kuondoa tofauti
za kimaendeleo kati ya ustawi wa kiwanda na jamii inayowazunguka”alieleza
Waziri Kairuki
Waziri aliutaka uongozi huo
kushiriki kimalilifu katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia kuboresha
miundombinu inayozunguka mazingira ya kiwanda ili kuendelea kushiriki kwa
vitendo na kuunga mkono jitihada za kuendelea eneo hilo.
Sambamba na hilo Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jumaa Abeld aliomba uongozi wa kiwanda
kuona namna ya kuchangia katika maendeleo ya eneo lao kwa kuchangia ujenzi wa
vyumba vya madarasa sita katika shule ya msingi ya Kitangwi pamoja na madarasa manne
katika shule ya msingi ya Kisemvule
zilizopo Wialya ya Mkuranga katika mkoa huo.
“Ombi letu ni kuona namna
kiwanda hiki kinavyoweza kuchangia katika maendeleo kwa kutujengea vyumba sita
vya madarasa katika shule zinazotuzunguka ili kusaidia uhaba uliopo na kusaidi
watoto wetu kujifunza katika mazingira mazuri,”alisema Jumaa.
Aidha Meneja Masoko wa
Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara aliahidi ifikapo Julai 05 mwaka huu uongozi wa
kiwanda utatoa taarifa za utekelezaji wa maombi hayo ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa 6.
“Tunaahidi kukutana kama
uongozi wa kiwanda ili kujadili na kutekeleza masuala ya msingi ikiwemo hili la
ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuendelea kuleta tija kwa uwepo wa kiwanda
katika eneo hili,”alisema Mwasara.
Naye, Meneja Fedha wa
kiwanda hicho Bi. Wema Mboga alishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha
mazingira ya wawekezaji nchini na kumpongeza ziara ya Waziri katika kutatua na
kuahidi kufanyia kazi masuala yaliyoelezwa kuwa ni changamoto kiwandani hapo
ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika, kutokamili kwa
leseni za uchimbaji kwa wakati, tozo kubwa za malighafi na kuongezeka kwa
gharama za uzalishaji kiwandani hapo.
AWALI
Kiwanda cha KNAUF
kilianzishwa mwezi Novemba mwaka 2015 kwa lengo la kuzalisha bidhaa za jasi (Gypsum board), gundi za jasi, pamoja na
chuma za jasi (metal profile) kufanya kazi na usambazaj.Kiwanda kinafanya
kazi katika nchi zaidi ya 80 ambapo katika nchi za kusini mwa Janga la Sahara,
Tanzania ni nchi pekee ambayo ina uwekezaji huo kutokana na sababu za mazingira
mazuri ya kibiashara na uwekezaji pamoja na sababu za kijiografia.Kampuni
imeajiri wazawa 150 katika Nyanja zote kwa kulenga ifikapo 2020 kiwanda kiweze
kuendeshwa na wazawa pasipo kutegemea wataalam kutoka nje.
=MWISHO=
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.