*Huzuni, simanzi, majonzi na vilio vyatawala mjini Morogorogo
HUZUNI, simanzi, majonzi na vilio vimetawala mjini Morogoro leo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwaakiongoza
 umati wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro, mkoani Morogoro katika 
mazishi ya wananchi waliofariki dunia kutokana na ajali ya moto wakati 
wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta 
kupinduka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 71 huku wengine 59 
wakijeruhiwa.
Mazishi
 hayo yameanza kufanyika leo (Jumapili, Agosti 11, 2019) katika eneo la 
makaburi la Kola Hill mjini Morogoro ambapo Waziri Mkuu amemwakilisha 
Rais, Dkt. John Magufuli. Ametoa pole kwa wafiwa wote na amewaomba 
wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.
Akizungumza na wananchi katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Msamvu mjini Morogoro iliyofanyika kwenye
 viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Waziri Mkuu ametumia fursa 
hiyo kuwashukuru viongozi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano 
waliouonesha wakati huu wa amajonzi.
Kufuatia
 ajali hiyo iliyotokea jana saa 2 asubuhi baada ya lori lenye shehena ya
 mafuta ya petrol kupinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu 
mjini Morogoro wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha 
pikipiki. Rais Dkt, Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya 
Kitaifa kuanzia jana Jumamosi Agosti 10,2019 na bendera zote 
zipeperushwe nusu mlingoti.
Mazishi
 hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
 Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi 
OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, 
Isac Kamwelwe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Waziri wa
 Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Wengine
 ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, Naibu Waziri wa Nishati, 
Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji 
pamoja na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, viongozi wa dini na 
wananchi wa mkoa wa Morogoro.
(mwisho)
 
 
 
 
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.