WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji
kutoka nchini Mauritius waje washirikiane na Watanzania katika uwekezaji
kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya utalii, viwanda vya sukari, nguo
na bidhaa za uvuvi.
Ametoa
kauli hiyo leo, (Jumatano, Agosti 28, 2019) wakati alipokutana na
kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar katika
Ukumbi wa Monyesho wa Pasfico Yokohama nchini Japan.
Waziri
Mkuu amesema nchi ya Mauritius ina uwezo mkubwa sana katika uzalishaji
wa sukari na wanayo nafasi kubwa ya kushirikiana na Watanzania katika
kilimo cha miwa na ujenzi wa viwanda vya sukari na Tanzania ina ardhi
nzuri na kubwa inayofaa kwa kilimo hicho pamoja na soko kubwa ndani na
nje ya nchi.
Amesema
uwekezaji katika sekta ya sukari utasaidia kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli za
kuhakikisha inamaliza tatizo la upungufu wa sukari nchini.
Akizungumzia
kuhusu sekta ya utalii, Waziri Mkuu amesema Mauritius imefanya vizuri
sana katika utalii na hasa ule wa kutumia fukwe za bahari. “Kwa vile
Tanzania inazo fukwe za bahari na maziwa naamini ushirkiano katika eneo
hilo utatuletea tija.”
Kuhusu
usafiri wa anga, Waziri Mkuu amesema kuwa wakati umefika sasa kwa
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuanza safari za kwenda Mauritius
ili kuvutia watalii wengi wanaokwenda Mauritius kufanya utalii wa
fukweni waje pia nchini.
Kuhusu
viwanda vya nguo, Waziri Mkuu amewahamasisha wafanyabiashara wa
Mauritius kuwekeza nchini hasa katika viwanda vya nyuzi za pamba na nguo
kwani Tanzania hivi sasa inazalisha pamba nyingi na yenye ubora wa
juu.
“Watanzania
wengi wameishia kuwekeza kwenye viwanda vya kuchambua pamba hivyo
wanalazimika kuuza pamba yao nje ya nchi na wenzetu Mauritius wameenda
mbali zaidi kwani wana viwanda vya nguo na viwanda vya nyuzi. Kwa sasa
Serikali ya Tanzania imeweka mkakati wa kujenda viwanda vya nguo ili
kuongeza tija.”
Amesema
kwa sasa wamekuabaliana na Waziri wa Mkuu huyo wa Mauritius
kuwakutanisha Mawaziri wa viwanda na Biashara wa Mauritius na Tanzania
wakae pamoja kwa ajili ya kufanya mazungumzo yenye lengo la kuwashawishi
wafanyabiashara wa Mauritius waje wawekeze katika viwanda vya nguo na
nyuzi nchini.
Kadhalika,Waziri
Mkuu amezungumzia kuhusu sekta ya Uvuvi, ambapo amesema Tanzania ina
eneo kubwa la bahari na maziwa linalofaa kwa uvuvi wa kibiahara na lina
samaki wengi lakini wanavuliwa kwa kiwango kidogo sana kutokana na
uwekezaji duni katika sekta hiyo.
Amesema
ingawa Serikali ya Awamu ya Tano inaandaa mazingira ya kufufa kampuni
za uvuvi nchini, bado nafasi ipo kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi hasa
nchini Mauritius kuja Tanzania kuwekeza kwenye uvuvi.
Kwa upande wake,
Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind ameihakikishia Serikali ya Tanzania
kuwa nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo na Wizara na Taasisi
zinazohusika na masuala ya uwekezaji nchini ili kupata taarifa za
kutosha zitakazomwezesha kuwashawishi wafanyabiashara wa nchi yake waje
wawekeze nchini.
Mazungumzo
hayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa
Afrika ya Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi na viongozi kutoka
Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.