Wednesday, December 14, 2016

MAVUNDE APOKEA TUZO YA MJASIRIAMALI WA KIKE-AFRIKA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Malkia Investment Ltd. Bi Jeniffer Shigole aliyeshinda Tuzo za wajasiriamali (African Enterprenership Award) nchini morocco kwa kuwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha Mazingira na Elimu kwa ubinifu wa bidhaa aina ya Elea Reusable Sanitary Pads na kujinyakulia dola 150,000/-. Kulia ni Meneja wa Programu wa Kampuni ya Malaika Investment Bw. Juma Rajabu. Tuzo hiyo iliwasilishwa katika Ukumbi wa Mikutano ya Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 14 Desemba, 2016
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akipokea Tuzo aliyoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu. Tuzo hiyo iliwwasilishwa katika Ukumbi wa Mikutano ya Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 14 Desemba, 2016.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.