Thursday, December 8, 2016

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KUSHEREHKEA UHURU WA TANZANIA BARA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, amewataka wananchi wote kushirikiana na kusherehekea uhuru wa Tanzania bara kwa kuunga juhudi za serikali ya awamu ya Tano ya kupinga ufisadi na rushwa nchini.
Kwa niaba ya serikali natoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hii kwa kuwakumbuka waasisi wetu waliotetea na kutuletea Uhuru wa nchi yetu. Aidha niwaombe wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kuimarisha uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu” amesema Mhagama.
Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza Miaka 55 ya uhuru ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo yetu”
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo atakuwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na,
Kitengo cha Mawasiliano serikalini
Ofisi ya Waziri Mkuu
TAREHE 08, DESEMBA, 2016.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.