Sunday, July 23, 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU MBOZI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kulia kwake) wakitazama Kimondo wakati walipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Mbozi mkoani Songwe Julai 23, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa  Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wa wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vwawa wilayani Mbozi Julai 23, 2017. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa  Wapili  kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Limdi, Erasto Zambi. 

 DED wa Mbozi, Elisey Mgoyi mmoja wa watendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Mbozi ambao Waziri Mkuu aliagiza wasimashwe kazi na wafanyiwe uchunguzi na TAKUKIURU.
DT wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Simon Noeli ambaye pia amesimamishwa kazi.
Cashier wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi  Bahati Chomoka pia amesimamishwa.kazi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe nje kidogo ya mji wa Vwawa mkoani Songwe Julai 23, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa wilaya ya Mbozi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kyalele wilayani humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama nguo za batiki  wakati walipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wa Mbozi kabla ya  mkutano wa hadahara uliohutubia wa Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nalyelye wilayani Mbozi, Februari 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.



EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.