Sunday, September 1, 2019

PROGRAMU YA KITALU NYUMBA YAWAPA HAMASA VIJANA KUSHIRIKI KWENYE SEKTA YA KILIMO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana walioshiriki katika mafunzo ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) katika Kijiji cha Ihemi alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya mafunzo hayo Mkoani Iringa.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bi. Lucy Nyalu akieleza jambo kuhusu ushirikishwaji wa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo walioshiriki katika mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Holly Green Bw. Octavian Laswai alipokuwa akikagua kitalu nyumba wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba, Mkoani Iringa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ihemi Bw. Antony Akata (wa pili kutoka kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea eneo hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
Muonekano wa Miche ya Nyanya iliyopandwa kwenye Kitalu Nyumba kilichopo katika Halmashauri ya Mafinga.
Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua na kuangalia miche ya Nyanya iliyopandwa kwenye kitalu nyumba (Green House). Kushoto ni Mmoja wa Vijana wanufaika na Mradi huo Bw. Ramadhani Haule.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akikagua Kitalu nyumba moja wapo kilichopo Ihemi, Mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Bi. Saada Mwaruka alipokuwa akikagua chanzo cha maji yanayotumika kumwagilia Kitalu nyumba hicho. (Katikati) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua miche ya Nyanya iliyopandwa kwenye trei maalumu alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.





EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.