Saturday, September 21, 2019

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAENDELEO YA MAFUNZO KWA VIJANA KUPITIA TEKNOLOJIA YA KITALU NYUMBA WILAYA YA CHAMWINO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Chamwino mara baada ya kuwasili katika wilaya hiyo kwa lengo la kutembelea maeneo yaliyojengwa Vitalu Nyumba “Greenhouse” na kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba, Wilaya ya Chamwino Septemba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Vumilia Nyamonga akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyojengwa Vitalu Nyumba “Greenhouse” na kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Godfrey Mnyande akitoa taarifa fupi kuhusu utekelezaji wa Programu ya Mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama. Programu hiyo inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Holly Green, Bw. Octavian Laswai (kushoto) akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Holly Green, Bw. Octavian Laswai (kushoto) akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Holly Green, Bw. Octavian Laswai (kushoto) alipokuwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House iliyojegwa katika Halmashauri ya Chamwino, Septemba 21, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Bw. Festo Masima ambaye ni mmoja wa vijana aliyenufaika na Mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) kuhusu ujuzi waliopata juu ya kujenga Vitalu nyumba hivyo.
Mwanagenzi mmoja wapo aliyenufaika na Mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) Bw. Fahdi Lyimo akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu bidhaa ya “Chill Source” iliyotengenezwa na Kikundi cha Vijana kiitwacho The One. Bidhaa hiyo imetumia kutengenezewa na Nyanya zilizovunwa na vijana hao katika Kitalu Nyumba kilichojengwa Halmashauri ya Chamwino. 


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.